AFUKUA MAITI YA MTOTO WAKE SIKU TATU BAADA YA MAZISHI, WANANCHI WACHOMA MOTO NYUMBA YAKE JIJINI MBEYA
Hili ndio Jeneza likiwa kwenye Gari ya Polisi kuelekea katika Hospitali ya Ifisi. |
Jeshi la Polisi wakiwa wamebeba Jeneza pamoja na watuhumiwa ambao wameusika katika kufukua Mwili huo |
Mara baada ya Polisi kuondoka nyumbani kwa mtuhumiwa wananchi waliteketeza kwa moto nyumba ya Luth.(Picha na Ezekiel Kamanga Mbeya)
|
Wananchi wakishuhudia tukio |
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Luth Segeleti (52)mkazi wa shigamba Mbalizi Wilaya ya Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya baada ya kufukua kaburi la mtoto wake kisha mwili kurudi nao nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya maombi ili afufuke.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema marehemu Baraka Mwafongo (22)alifariki February 15 na mazishi kufanyika Februari 16 mwaka huu, lakini mama Mzazi Luth Segeleti anayeabudu Kanisa la Ufufuo na Uzima alidai mwanawe atafufuka siku ya tatu.
Kidavashari amesema kuwa Luth alianza zoezi la ufukuaji saa sita usiku na kumaliza zoezi hilo mapema alfajiri kwa kushirikiana na vijana wawili akiwemo mwanawe.
Aidha aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda nao nyumbani kwake kisha kuogesha na kuupaka mafuta tayari kwa maombi.
Hata hivyo baadhi ya majirani walimtilia shaka Luth baada ya kumkuta na jembe akiwa ametoka makaburini na walipomuuliza alikiri kufukua na kudai kuwa mwanawe hajafa hivyo atafufuka baada ya maombi.Wananchi walitoa taarifa Polisi ambao walifika eneo la tukio na kumhoji Luth ambapo alikiri kufukua kaburi la mtoto wake hivyo Polisi walichukua jeneza tupu na mwili kuupeleka hospitali teule ya Ifisi kwa uchunguzi zaidi.
Mara baada ya Polisi kuondoka nyumbani kwa mtuhumiwa wananchi waliteketeza kwa moto nyumba ya Luth ambapo Jeshi la Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi wakiongoza na mkuu wa Polisi Wilaya hiyo Debora Mrema kufanya kazi ya ziara kuzima moto huo.
Baadhi ya watu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo la uchomaji moto.
No comments:
Post a Comment